Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran: Msimamo wa India.

Kujiondoa kwa Marekani kwenye mpango wa utenda kazi (JCPOA) mnamo Mei mwaka wa elfu mbili kumi na nane na kurejesha vikwazo dhidi ya kampuni za mafuta za iran tarehe sita Agosti kumeimbua kwa mara ingine swala la Iran la nyuklia katika jukwaa la ulimwengu. Ingawa wanachama wengine katika mpango huo kama vile Uingereza, Ufaransa, Urusi, China na Ujerumani wameshikilia kujituma kwao katika mpango huo hadi sasa, mataifa hayo yanashinikizwa na Marekani kujiondoa  na kusitisha ushirika wa kiuchumi na Iran.

India ina uhusiano mkubwa na Iran katika nyanja tofauti kama vile ushirika wa kisiasa, uchumi na stratejia. Ushirika wa India na Iran katika sekta ya kawi ni wakaribu mno, huku Tehran iikiwa inaisambazia India angalau asilimia saba ya mafuta ya India kutoka nchi za nje. Iran ilishikilia nafasi ya tano katika orodha ya nchi zinazouzia India bidhaa za mafuta,ikiwa inafuata Saudi Arabia, Iraq, Australia na Nigeria. Zaidi ya hayo, India na Iran zimeendeleza uhusiano wa kisiasa huku Waziri Mkuu Narendra Modi  akitembelea nchi hiyo mnamo mei mwaka wa elfu mbili kumi na sita, na kasha Rais wa Iran Hassan Rouhani akaitembelea India mnamo Februari mwaka huu.

India na Iran zililitia sahihi mikataba wa kuendeleza bandari ya Chabahar ambayo iko katika gumba ya Persian mnamo Mei mwaka wa elfu mbili kumi na tano. Wakati wa ziara yake Waziri Mkuu Narendra Modi, makubaliano yaliafikiwa kati ya nchi za Iran, Afghanistan na India ili kutumia Bandari hiyo ya Chabahar kama njia ya kusafirishia bidhaa kutoka India hadi Afghanistan. India vile vile imeashiria nia yake yakuhusika katika oparesheni za Bandari hiyo huku Iran ikiwa na mipango ya kutafuta makampuni ya kimataifa ili kuendeleza oparesheni katika bandari ya Chabahar.

Baada ya Rais wa Marekani kutangaza kujiondoa kwa nchi yake kwenye mpango wa utendakazi wa JCPOA, wizara ya Maswala ya nje ya India ilisema kuwa uhusiano wa India na Iran hautegemei nchi yoyote ingine. Hata hivyo, wakati wa ziara yake nchini India, mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Bi. Nikki Healey aliitaka India kusitisha uagizaji wa mafuta kutoka Iran.

New Delhi imezidi kushikilia kwamba uamuzi wowote unaohusu kukatiza mafuta kutoka Iran utazingatia matakwa ya India ya kawi na usalama. Mwezi jana, Waziri wa Maswala ya nje ya dola Jenerali V K Singh alisema kuwa India inafuatilia kwa making maendeleo yanayoweza athiri maslahi ya Taifa ikiwa ni pamoja na usalama na kawi. Waziri huyo aliongeza kuwa India itachukua hatua zinazo faa ili kulinda maslahi yake.

Hali inayotokana na kujiondoa kwa Marekani kwenye mpango wa JCPOA N kurejeshwa kwa vikwazo dhidi ya iran ni swala nyeti kwa diplomasia ya india. Huku ikiwa wazi kuwa India inathamini ushirika wake na Iran, New Delhi italazimika kufanya maamuzi yenye kuzingatia mwonekano mkuu wa kisiasa wa nafasi ya India katika mpango wa dunia unaozidi kubadilika.