Msisimuko wa baada ya tetemeko la ardhi wazua hofu baada ya tetemeko la ardhi nchini Indonesia. 

Msisimuko wa ardhi wenye nguvu ulikumba kisiwa cha Lombok nchini Indonesia siku ya Alhamisi na kuzua hofu miongoni mwa manusura wa tetemeko la ardhi lililokumba kisiwa hicho na kupelekea vifo vya zaidi ya watu mia moja sitini na wanne. Manusura hao walikuwa wakisubiri usaidizi kwa siku nne baada ya mkasa huo kutokea. Msemaji wa idara ya majanga ya Indonesia Sutopo Purwo Nugroho alisema kwamba kumekuwa na misisimuko mia tatu hamsini na tano tangu siku ya Jumapili.