Bunge la India la pitisha mswada wa matabaka yaliyotelekezwa. 

Bunge la India limepitisha mswada wa mwaka wa elfu mbili na nane wa kuzuia dhuluma dhidi ya matabaka yaliyotelekezwa katika jamii, almaarufu kwa kimombo kama ‘Scheduled Castes’. Huku akichangia mjadala juu ya mswada huo kwenye bunge la Rajya Sabha, Waziri wa haki za kijamii Thaawar Chand Gehlot alisema kuwa serikali imejitolea katika kulinda maslahi ya maskini pamoja na Dalits. Waziri huyo aliongeza kuwa mswada huo unatoa nafasi ya kuunda mahakama spesheli za kushughulikia kesi zinazofungamana na dhuluma dhidi ya matabaka yaliyotelekezwa katika jamii.