Usaidizi kwa wanawake wanaotelekezwa na mabwana wanaoishi ughaibuni waongezwa hadi dola elfu nne kwa kila kesi.

Wizara ya Maswala ya Nje imeongeza kiwango cha usaidizi wa kisheria na fedha kwa wanawake wa India wanaotelekezwa na mabwana zao wanaoishi katika nchi kumi na tatu za ughaibuni. Kiwango hicho kimeongezewa hadi dola za Marekani elfu nne kwa kila kesi. Waziri wa Muungano V K Singh aliambia bunge la Rajya Sabha siku ya Alhamisi kwamba sera za hazina ya maslahi ya jamii ya wahindi zilifanyiwa utathmini kwa nia ya kuwasaidia wanawake ambao wameolewa na Wahindi wanaoishi ughaibuni. Hapo awali, kiwango hicho kilikuwa kisichozidi dola elfu tatu kwa kila kesi katika mataifa yaliyoendelea na dola elfu mbili katika mataifa ambayo yangali yana kua.