India inaunga mkono juhudi zote kwa amani, upatanisho nchini Afghanistan

Serikali ya India inasema, inasaidia jitihada zote za amani na upatanisho nchini Afghanistan ili kuhifadhi umoja na wingi na kuleta usalama, utulivu na ustawi wa nchi hiyo.
Msemaji rasmi alisema huko New Delhi kuwa India inafahamu kwamba Shirikisho la Urusi linashiriki mkutano juu ya Afghanistan huko Moscow leo.
Msemaji huyo alisema, sera ya uwiano wa India imekuwa kwamba jitihada hizo lazima ziongozwe na Afghanistan, na kudhibitiwa na Serikali ya Afghanistan.