India Na Turkmenistan Yaimarisha Ushirikiano

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo ya nje wa Turkmenistan Rashid Meredov, alitembelea India kwa muda mfupi na alifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa India Dk. S. Jaishankar. Viongozi hao wawili walijadili masuala ya nchi mbili na ya kikanda. Waziri wa Mambo ya nje wa India alielezea kuwa majadiliano hayo yaliangazia uunganisho wa maswala ya kikanda.

Turkmenistan ni moja wapo ya jamhuri tano za Asia ya Kati, ambayo ilipata uhuru mapema miaka ya 1990 kutoka kwa USSR ya zamani. India inazingatia Asia ya Kati kama jirani wake. Eneo la kipekee la kijiografia la Turkmenistan katika kanda linaifanya iwe nchi yenye umuhimu katika mashirikiano kati ya kikanda. Nchi hiyo inaunganisha Asia ya Kusini, Asia ya Kati na Asia ya Magharibi pamoja, kama majirani wake, Afghanistan kusini mwake na Irani katika magharibi . Majirani zake za Asia ya Kati ni Kazakhstan na Uzbekistan. Turkmenistan ina pwani ya Bahari ya Caspian na hii hutoa lango la Eurasia na Ulaya. Kuboresha mbinu za usafiri imekuwa kipaumbele cha Turkmenistan. Katika mwaka wa 2016, nchi ilijenga moja ya viwanja vya ndege kubwa katika kanda hilo na gharama ya karibu dola bilioni 2.3 za Amerika.

Kwa idadi ya watu, Turkmenistan ni nchi ndogo na watu wapatao milioni 6 lakini inabeba kiwango kikubwa cha uchumi. Inayo akiba ya gesi asilia iliyodhibitishwa kuwa nambari nne kubwa duniani. Ni tajiri pia katika mafuta, sulphur na madini mengine. Benki ya Dunia inakadiria GDP yake kuwa karibu dola bilioni 40.5 za Amerika. Utawala wa Rais Gurbanguly Berdimuhamedov unajaribu kutofautisha uchumi na kumekuwa na ulenga wa sekta za jadi kama vile mafuta na gesi, kilimo, ujenzi, usafirishaji na mawasiliano na pia juu ya kuongeza shughuli katika sekta mpya kama vile kemikali, mawasiliano ya simu na teknolojia zingine za hali ya juu. Turkmenistan pia inatekeleza mpango wa uchumi wa dijitali ya 2019-2025 kwa njia ya awamu.

Turkmenistan inafuata sera ya ‘kutokubalika kwa upande wowote’ katika ushirika wake na ulimwengu. Sera hiyo pia imeidhinishwa na Mkutano Mkuu wa UN katika mwaka wa 1995. India ilikuwa mdhamini mwenza wa Azimio hilo na kwa sasa Ashgabat inaadhimisha kumbukumbu yake ya 25.

Kwa sababu ya eneo lake la kipekee la kijiografia na matarajio ya kiuchumi, Turkmenistan inaweza kuchukua jukumu muhimu katika ushiriki wa India na Asia ya Kati. Nchi hizo mbili zinashiriki uhusiano mrefu wa kihistoria na kiutamaduni tangu jadi. ‘Njia y Silk’ ambayo ni maaruu iliunganisha nchi hizi mbili. Uhusiano uliendelea kuwa na nguvu wakati wa kipindi cha enzi kwani watakatifu na wasomi kutoka eneo hilo walikuwa wanatembelea India. Shah Turkman Bayabani alikuwa mtakatifu maarufu wa Sufi, ambaye aliishi India katika karne ya 13. ‘Turkman Gate’ ilioko jijini Delhi ilijengwa kwa heshima yake katika karne ya 17. Mshauri wa Mfalme Akbar, Bairam Khan alikuwa wa asili ya Turkmen.

Uhindi na Turkmenistan wanafurahia uhusiano mzuri wa kisiasa na kitamaduni. Kumekuwa na ziara nyingi katika ngazi za juu za kisiasa kati yao . Rais Gurbanguly Berdimuhamedov alitembelea India mnamo Mei 2010. Waziri Mkuu Narendra Modi alitembelea Turkmenistan mnamo Julai 2015 na MoU kadhaa muhimu na makubaliano yalitiwa saini. Kituo cha Tiba ya Jadi na Yoga pia kilizinduliwa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake mnamo 2015.

Licha ya uhusiano wa kindani na mtazamo wa watu kwa watu wenye nguvu, uhusiano wa kiuchumi wa nchi mbili haujafanikiwa bado.Katika mwaka wa 2018-19 biashara yao ilikuwa karibu dola za Marekani milioni 66. Ukosefu wa habari sahihi juu ya fursa zinazopatikana kwa pande zote mbili na kutokuwepo kwa usafirishaji wa moja kwa moja wa ardhi kati ya India na Asia ya Kati huzingatiwa kati ya vizuizi vikuu. Migogoro nchini Afghanistan pia imekuwa shida kubwa katika uhusiano wa Asia Kusini na Asia ya Kati. Nchi zote mbili zimekubaliana kuja pamoja ili kuleta amani na utulivu nchini Afghanistan.

Hata hivyo, maendeleo ya hivi karibuni yanaibua matarajio ya kuongeza zaidi uhusiano wa nchi hizi mbili. India inawekeza katika bandari ya Chabahar ya Iran. Turkmenistan na Kazakhstan tayari zina kiungo cha reli kwenda Irani. Kuunganisha bandari ya Chabahar na mtandao wa reli ya Irani itaboresha uunganisho wa India na Turkmenistan na Asia ya Kati. Katika mwaka wa 2018, India ilijiunga na Mkataba wa Ashgabat, ambao unaunda usafiri wa kimataifa na usafirishaji kati ya Irani na Oman kutoka Asia Magharibi na Turkmenistan na Uzbekistan kutoka Asia ya Kati.

Vivyo hivyo, hivi karibuni maendeleo yamefanywa kwenye bomba la gesi asilia lililokusudiwa la Turkmenistan-Afghanistan-Pakistan-India (TAPI). Makubaliano ya Uuzaji na Ununuzi yalitiwa saini mnamo 2012. Turkmenistan iliripoti kwamba ujenzi wa TAPI katika maeneo yake ni kama ilivyo kwa ratiba na katika mwaka wa 2018, ujenzi nchini Afghanistan ulizinduliwa. Uhusiano wa pande mbili wa Indo-Turkmen unatarajiwa kupanuka katika siku za usoni.