Waziri mkuu wa India bw Modi atazindua  mkutano wa kila  mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mnamo tarehe 23 ya mwezi wa Mei

Waziri Mkuu wa India bw Narendra Modi atazindua Mikutano ya kila Mwaka
ya Benki ya Maendeleo ya Afrika  mnamo tarehe 23 ya mwezi huu. Wakati
alipokuwa akizungumzia na vyombo vya habari katika mji wa  New Delhi,
Katibu wa wizara ya mambo ya Uchumi ya India bw Shaktikanta Das
alisema, ni mara ya kwanza katika historia ya AfDB Group kwamba nchi
ya  India itafanya  mkutano mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika .
Alisema, mkutano huo  utafanyika kutoka  tarahe 22 hadi 26  ya mwezi
wa Mei katika mji wa Gandhinagar, katika jimbo la India la  Gujarat.
bw  Das alisema, mikutano ya kila mwaka ni tukio kubwa ya Bank, ambayo
kushuhudia  wajumbe 3000 kutoka nchi wanachama 81 kutoka dunia nzima.