Yemen Imo Katika Hatari ya Njaa Mbaya Zaidi Duniani kwa Miongo: UN.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa Yemen iliyokumbwa na vita iko katika hatari ya karibu ya njaa mbaya zaidi ambayo ulimwengu haujashuhudia katika miongo kadhaa. Antonio Guterres jana alisema kuwa kwa kukosekana kwa hatua ya haraka, mamilioni ya maisha yanaweza kupotezwa. Nchi ambayo imevumilia vita vya miaka mitano kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na vikosi vya serikali.

Onyo la Guterres linakuja wakati Marekani inatishia kuorodhesha kundi la Houthi kama sehemu ya kampeni yake kubwa ya shinikizo dhidi ya Tehran.

Wafanyikazi wa misaada wameelezea hofu kuwa hatua hiyo itazuia misaada ya kuokoa maisha kufika nchini na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi nchini Yemen.