Kiwango cha Kupona cha COVID-19 cha India Kimeboreka Hadi Asilimia 96.51.

Kiwango cha kupona cha COVID-19 sasa kimeboreshwa hadi asilimia 96.51. Jumla ya wagonjwa 17,817 wa COVID walipona katika masaa 24 yaliyopita. Jumla ya marejesho yamepanda hadi zaidi ya millioni kumi laki moja na elfu 29. Wizara ya Afya ilisema, kesi ya waliolazwa hospitalini kwa sasa yanajumuisha asilimia 2.04 tu ya jumla ya visa vya wagonjwa. Hivi sasa, jumla ya kesi za wagonjwa nchini ni laki mbili 14 elfu 507.

Katika masaa 24 yaliyopita, kesi 15,968 ziliripotiwa na kuchukua jumla ya idadi ya wagonjwa nchini hadi zaidi ya milioni kumi laki nne na elfu 95. Wizara ilisema, kwa sasa, Kiwango cha vifo wa Kesi nchini India ni kwa asilimia 1.44, ambayo ni moja ya chini kabisa ulimwenguni. Wakati wa masaa 24 iliyopita, vifo 202 viliripotiwa kuchukua takwimu hadi laki moja 51 elfu 529.