Wahindi waliopotea labda katika  jela la Badush huko nchi ya Iraq, anasema hayo Bi  Sushma Swaraj

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa India bi  Sushma Swaraj na Mawaziri
wa Nchi kwa Masuala ya Nje bw MJ Akbar na bw VK Singh siku ya Jumapili
walikutana na familia za Wahindi 39 ambao wamepotea nchini Iraq tangu
mwaka 2014. wakizungumza juu ya watu wasiopo, Bi Swaraj alisema,
vyanzo vya Iraq vimeambia bw  VK Singh kwamba Wahindi wasiojulikana
walipo huenda labda wamefungwa jela huko Badush ambako vita
vinaendelea.