Waziri Mkuu wa India bw Modi amesihi serikali za majimbao ya India kuchukua hatua kali dhidi ya waangalizi wa ng’ombe waliohusika katika ghasia

Waziri Mkuu wa India bw  Narendra Modi siku ya Jumapili alisema hatua
kali inapaswa kuchukuliwa dhidi ya watu ambao wanahusika katika vurugu
kwa jina la ulinzi wa ng’ombe. Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Bunge
bw Ananth Kumar, Waziri Mkuu pia alisema kuwa serikali za majimbo
zinapaswa kuchukua hatua dhidi ya watu hao. Waziri Mkuu wa India bw
Narendra Modi alisema, kuna sheria za kulinda ng’ombe lakini kuchukua
sheria katika mikono yao  haikubaliki. Bw Modi alisema, kuna jaribio
la kutoa rangi ya kisiasa na ya jamii kwa masuala kama hayo ambayo
hayatafaidika  kwa nchi. Waziri Mkuu wa India bw  Narendra Modi pia
alisihi vyama vya siasa kuja pamoja  kwa kupambana na rushwa.