BIMSTEC MINISTERIAL MEET KATIKA KATHMANDU

Mkutano wa 15 wa mawaziri wa BIMSTEC wakamilika mjini Kathmandu Nchini Nepal hivi jana. Akifunguwa Mkutano huo kiongozi wa nchi ya Nepal Bwana Sher Deuba alisema kuwa anamatumai kuwa mwisho wa mkutano huo utaleta nchi hizo chama kuwa rafiki wa karibu ilikuongeza Ushirikiano baina yao. Waziri mkuu bwana Deuba pia alijadilia maswala kadha yanayokumba nchi chama kwa ujumla kama vile swala la ukuwaji wa ugaidi katika nchi chama, Usafirishaji wa silaha bila vibali na usafirishaji wa dawa za kulevya. 
 
Bi Sushma Swaraj waziri wa mambo ya nje wa nchi ya India aliongoza wajumbe wengine kutoka serikali kuelekea nchini Nepal kama mwakilishi wa serikali ya nchi ya India. Bi Sushma Swaraj pia aliweza kuwa na mikutano na mawaziri wengine wa nje wa nchi Jirani kama Nepal na Bhutan.
 
Katika Mkutano wa BIMSTEC Nchi chama ni India, Nepal, Bhutan, Bangladesh, Sri lanka, Myanmar na nchi ya Thailand. Kwa maswala waliojadiliana ni kama vile Ukuwaji wa Economia ya nchi hizo, Biashara, uwekezaji, Nishanti, Tabia Nchi, Ugaidi na ukulima na nyinginezo.