Waziri Mkuu wa India Bw Modi, Waziri Mkuu wa Japani Bw  Shinzo Abe kuweka jiwe la msingi kwa treni ya risasi leo

Waziri Mkuu wa India bw Narendra Modi na mwenzake wa Japan, Bw Shinzo
Abe, leo wataweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa treni ya kasi
kati ya mji wa  Ahmedabad na mji wa Mumbai.  Treni itafunika umbali wa
zaidi ya kilomita 500 kwa saa mbili. Mradi huo unatarajiwa kukamilika
mpaka mwaka wa 2022. Japani imeongeza mkopo mzuri kwa mradi wa kitovu
uliofikiriwa na Bw Modi. Waziri Mkuu wa India bw Modi na Waziri Mkuu
wa Japan  bw Abe  pia walitembelea Msikiti wa Sidi Saiyyed wa karne ya
16 jioni na walifurahia utendaji wa chombo cha muziki .