Uhusiano ulioko kati ya India na nchi za ASEAN unaendelea kuongezeka

Ushiriki wa India na ASEAN katika eneo jipya la Indo-Pasifiki limepata kasi zaidi kufuatia utaratibu wa ‘Sera ya Mashariki ya  Waziri Mkuu wa India Bw Narendra Modi katika Mkutano wa 12 wa ASEAN-India na Mkutano wa 9 wa Mashariki mwa Asia mnamo Novemba mwaka 2014.ushiriki huu wa nne ni muhimu kwa Waziri Mkuu wa India Bw Modi  .

Katika Mkutano wa 15 wa ASEAN-India huko Manila, Mheshimiwa Modi na Waongozi wa ASEAN walipitia shughuli za kukumbusha zilizofanyika mwaka 2017 ili kuashiria miaka 25 ya ushirikiano wa mazungumzo wa India na ASEAN na wigo mpana wa ushirikiano wa ASEAN-India katika nyanja zote.

India na ASEAN zina taratibu za mazungumzo 30 ambazo hukutana mara kwa mara, pamoja na Mikutano 7 ya Waziri katika Mambo ya Nje, Biashara, Utalii, Kilimo, Mazingira, Nishati Yenye Kuwezesha na Mawasiliano.