HISTORIYA YA USHIRKIANO KATI YA NCHI YA INDIA NA BARA LA AFRICA

Kila mara nchi ya India imekuwa mshirika mkubwa wa bara la Africa kwa jumla  .

Tangu karne nyingi zilizopita  wanaoishi hizi mbili wamekuwa na mshikamano dhabiti.Tukiangalia nyuma kidogo katika historiya ,tunaona kwamba hata kabla ya Vasco Da Gama kutambua njia ya majini inayoelekeza India kupitia mji wa cape of Good Hope , kabla ya hayo jamii za Wahindi na wenye kuishi mashariki mwa bara la Africa walikuwa na uhishiano mwema . Akiolijia yaelezea kwamba mara ya kwanza ambapo wahindi walipata fursa ya kuonana na waafrica ilikuwa kwenye bonde la Nile  ambapo ustaarabu ulianza mapema katika karne nne kabla ya yesu kuzaliwa . Baadaye katika enzi ya babyloniani biashara nje ya India zilienezwa hadi katikati mwa Misri , Kusema kweli ushirkiano  kati ya wababeloni na waharappani uliokuwepo hata kabla ya miaka elfu mbli na mia tatu ya yesu kuzaliwa . Ni jabo amablo limekuwa wazi baada ya uchmbuzi wa kiakiolojia uliofanywa  katika eneo la Lathal karibu na mji wa Ahmedabad humu India ,Pia inajuliwa kuwa makasisi wa zamani kutoka Misri walikuwa wakipata kutoka India mimea yenye manukato walioichoma katika ibada kama ubani . Herodotust mwana historia mahsuhuri wa zamani alieleza   mengi yanayohusu bidhaa zilizoagizwa na misri zaidi ya hayo memea na mafuta yenye kunukia ambapo India ndio ilikuwa kituo maalum cha biashara hiyo , Uchimbuzi wa hivi karibuni umeonyesha wazi kwamba vifaa vilivyotumika kuuda utamaduni wa marembo nchini misri kitovu cha bidhaa hizo kilikuwa India,kusema kweli bidhaa hizi ziliangizwa na wamisri kwa gharama ya juu kutoka huko India kupitia kwao wafanya biashara wa kiarabu na Mesopotamia liliwapa nafasi njema ya kuimarisha uhushiano na jamii za humu Inidia. Lakini polepole hadi mwakani wa kumi na tano kabla ya yesu kuzaliwa Misri ilianza kuwa kituo maalu cha biashara ya baharini licha ya hayo kituo pekee za kukutania kati ya watokaa mashariki na magharibi .  Hakika ni kwa ajiri ya misri , India ilipata kuhamasisha nyanja za kiuchumi na mataifa ya magharibi.

UHUSIANO WA BIASHARA KATI YA NCHI YA INDIA NA BARA LA AFRICA

Wakati huu nchi ya india inaendelea kunufaisha uhusiano wake wa kiuchumi na nchi za Bara la Africa , licha ya hiyo nchi ya india inaongeza ushirkiano kati ya watu wa pande zote mbili . Mkutano wa tatu wa India na Africa ambao ulifanyka mnamo mwezi wa oktoba mwaka elfu mblili kumi na tano , ulisadia kuongeza uhusiano kati ya india na bara la Africa . Nchi ya india ilitumia nafasi hii kwa kuimarisha diplomasia na uchumi . Mkutano huo uliongeza uhusiano katika maeneo ya kibiashara na uwekezaji kati ya pande zote mbili .Hata sekta ya binafshi pia ilishiriki katika mkutano huo . viongozi wengi wa nchi za bara la afrika hasa kutoka nchi zinazoendelea walishiriki katika mkutano huo . Malengo ya mkutano huo yalikuwa kunufaisha uhusiano kati ya india na nchi za bara la africa katika sekta nyingi kama vile biashara ,uwekezaji , usalama wa chakula , tecknologiya za mawasiliano na habari , amani na usalama, na utawala mzuri. viongozi wa nchi ya india na bara la africa walikubali umuhimu wa mawasiliano kati ya watu wa pande zote mbili.

Biashara kati ya India na bara la afrika liliongeza kutoka dolla za marekani bilioni ishirini na tano mnamo mwaka elfu mbili na saba na lilifikia doll za marekani bilioni hamsini na saba mnamo mwaka elfu mbili kumi na moji,  mpaka mwaka elfu mbili kumi na tatu bihashara hizo kati ya pande zote mbili lilifikia dola za marekani sitini na saba . Kuna Makadario kwamba biashara kati ya pande zote mbili zitafikia dolla za marekani bilioni themanini mpaka mwaka elfu mbili na ishirini. Serikali ya inida ilifanya mpango wa bara la africka mnamo mwaka elfu mbili na mbili , lengo ya mpango huo ulikuwa kuongeza biashara kati ya pande zote mbili , kipindi cha mpango huo ulikuwa kutoka mwaka elfu mabili na mbili hadi elfu mbili na saba na kuhushisha nchi ishirini na nne za bara la africa katika mpango huo, sasa mpango unatoa faida za kibashara kati ya pande zote mbili. Serikali ya India inafahamu umuhimu wa nchi za bara la afrika na shirika la BRICS lenye nchi za (Brazil ,Russia , India, China. South Africa)  ni mfano wa kidiplomasia baina ya nchi ya India, Brazil na Africa kusini yatasadia jitihada za india za kutaka kuwa nchi mwanachama kudumu katika baraza la usalma la umoja wa mataifa na nchi za bara la africka zitasadia sera ya india katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.