WANAFUNZI KUTOKA BARA LA AFRICA NCHINI INDIA

Uhushiano kati ya India na Bara la Afarica in mkongwe na tena wa kisasa. Ukongwe wake unatokana na ukweli kwamba nchi nyingi katika bara la Afirika , zilikuwa chini ya nira ya mkoloni . Jinsi ilivyokuwa india ,hadi hapo zilipojikinaswa kutoka utawala huo wa kegeni baada ya harakati za kupigania uhuru. Usasa wake ni kwamba , baada ya kujipatia uhuru , nchi hizo zimejikuta zina majukumu sawa ya kuleta maendeleo na kuendeleza ushirkiano kwa manufaa ya kila upande , kwenye mfumo ambao kanuni zake zinabadilika kila kukicha. Mambo hayo ndiyo chimbuko la uhusiano kati ya india na nchi na bara la Africa.

Lakini ni dhahiri kwamba wachambuzi wa mambo yanyozileta pande hizi mbili pamoja wamekuwa wakiyatilia uzito mkubwa ya kisiasa na kiuchumi na kulisahau mojawapo muhimu ambalo ni utamaduni . Idadi kubwa ya wanafunzi wa  kiafrika wanoosomea hapa inida ni sehemu kubwa ya ushirkiano wa kitamaduni.

kulingana na makisio yasiyothibitishwa , takriban wanafunzi wa kegeni wapatao elfu  kumi kutoka kila pande la dunia huja nchini India Kujiendeleleza ,pia sehemu fulani inatoka mataifa yaliyopiga hatua kubwa kimaendeleo . jambo la kuvutia ni kwamba idadi kubwa ya wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea huja hupa nchini kuchukua masomo katika fani mbali kame vile historia .falsaha.siasa , uchumi, uhandishi na teknolojia, madawa , syansi ya komputa , teknolojia ya habari na mambo yahusuyo ukusanyaji na usambazaji wa habari.

Lakini wanafunzi kutoka nchi zilizopiga hatua kubwa kiviwanda huja nchi ni india kujifunja muziki na densi za kienyeji  pia lugha ya kihindi. Kati ya wanafunji wanaotoka nchi zilizoendelea  , asilmia arobaini hadi hamsini ni kutoka bara la Afrika , ikiwemo Afrika mashariki na kati. Sababu moja wapo inayowafanya wanafunzi hao kuja nchini India kujiiendeleza kimasomo jinsi walivyomweleza mwandishi wetu , ni kwamba kuna ule uhuru wa kidemokrasia unaopatikana kwenye vyuo vya hapa nchini. Sababu nyingine muhimu in kwamba gharama ya masomo hapa Inida ni nafuu  kuliko zinazotozwa wanafunzi wanavyochukua mafunzo sawa na hayo katika mataifa yaliyoendelea.

Isitoshe, India kwa ajili ya kuendeleza uhusiano wake mkongwe na nchi za bara laAfrka ,hutoa nafasi za bure za masomo kwa idadi fulani ya wanafunzi kutoka bara hilo jambo linakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hao. Halimashuhuri ya india inayoshughulikia mambo ya utamaduni na nchi za kigeni ambayo ipo chini ya wizara ya Mashauri ya kigeni , ila tu hujiendesha shughuli zake yenyewe , husadia wanafunzi kupata nafasi kwenye vyuo vikuu na kupanga jinsi watakavyohdumiwa wakiwa humu nchini , Isitose, halmashauri hiyo hupatina habari zozote muhimu kuhusu fani mbalimbali za masomo yanayotolewa na serikali ya india . pia kuna mipango ya masomo ambayo huwapatia wanafunzi fursa ya kujiendeleza upande wa fani za kiufundi kwa ufupi.

Vyuo kadha vya hapa nchini vinavyotoa mafunzo ya juu in kama vile chuo kikuu cha Delhi , Kolkata, Mumbai,Pune , Punjab , Roorkee, Banglore, Jawarlala Nehru na chuo cha fundi cha India (IIT) na kadhalika . zina afisa maalum anayeshugulikiya maslahi ya wanafunzi wa kigeni kwa upande mmoja na wizara ya mashauri ya kigeni na afisi za ubalozi wa India katika Nchi za kigeni.