Benki kuu ya Dunia imetangaza  dola za Marekani bilioni 57 kwa Afrika kusini mwa Sahara

Benki kuu ya Dunia imetangaza dola za Marekani bilioni 57  kwa ajili
ya Afrika kusini mwa Sahara zaidi ya miaka mitatu wa fedha. Dola za
marekani bilioni 45 zitakuja kutoka Chama cha Maendeleo ya Kimataifa,
mfuko wa Benki ya Dunia ambayo hutoa misaada na mikopo ya riba ya bure
kwa ajili ya nchi maskini zaidi duniani.  Rais wa Benki kuu ya Dunia
bw Jim Yong Kim katika taarifa yake  jana alisema kuwa dola za
marekani bilioni 8  zitapatikana kutoka  sekta binafsi .