Sekta za Afya Na Matibabu Katika Nchi Ya India

Sekta ya afya inatarajiwa kukuwa kwa dola za marekani bilioni mia mbili na themanini mpaka mwaka elfu mbili na ishirini . Sekta hiyo inapata ukuaji kila mwaka, asilmia kumi na sita lakini ripoti ya shirika la FICCI-KPMG inasema kwamba sekta hiyo ya afya inahitaji sera maaluma na miundobinu ili watu wa india wanaweza kupata huduma bora ya afya.

kiwanda cha afya kinataka ukuaji muhimu na wafanyakazi katika sekta hiyo wanatarajiwa kuwa milioni 7.4 mnamo mwaka elfu mbili ishirini na mbili – kwa mujubu wa ripoti hii ya sektya hiyo ya afya ilikuwa takriban bilioni sabini na tatu nukta tisini na mbili mnamo mwaka elfu mbili kumi na moja na inatrajiwa kupata ukuaji asilmia kumi na sita takriban dola za marekani bilioni mia mbili na themanini mpaka mwaka 2020.

Ripoti hiyo iliongeza kwamba huu ni wakati kwa serikali kutambua umuhimu wa sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo ni nafasi ya maendeleo sio tu kwa majibo ya taifa bali pia kwa taifa kwa jumla .

Kutokana na kuongezeka kwa magonjwa , sekta ya afya nchini india inahitaji sera maalum na miundombinu . Hatua ya miundombinu sio tu kusaida sekta hiyo bali pia kupokea uwekezaji mkubwa na kupungua gharama ya huduma za afya.

Ripoti hiyo inaendelea kusema sekta ya afya nchini india inatazamiwa kama sekta ya kijamii na serikali inatoa bajeti dogo kwa sekta hiyo.

Hivi sasa serikali ya India inatumia asilmia 4.2  tu kwa mapato ya mwaka ya taifa  (GDP) juu ya sekta ya afya na asilmi 1 tu inachangiwa na sekta ya umma ambayo ni ndogo mno miongoni mwa nchi nyingine za dunia

Ripoti hiyo ilieleza kwamba sekyta ya afya ni sekta kubwa nchini india inayotoa ajira mno na sera maalu inaweza kuongeza ajira zaidi katika sekta hiyo. Wafanyakazi katika sekta ya afya wanatarajiwa kuwa milioni 7.4 mnamo mwaka 2022 kutoka milioni 3.6 mnamo mwaka 2013 .

Hisa ya uwekezazi moja kwa moja kutoka nje  tangu mwaka 2011 uliongezeka maradufu na hali hii inaonyesha kwamba wawekezaji wa kigeni wanaoyesha hamu kubwa katika sekta hiyo nchini Inida, Nafasi za uwekezazi zimeongezeka katika sekta ya afya ya India na sekta ya afya inavutia makampuni ya kigeni .

Ripoti ya FICC-KPMG ilisema kwamba utalli ya matibabu umekuwa sekta maalum kutokana na ukuaji wa sekta ya afya nchini India.

Watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanakuja nchini India kwa faida ya gharama za matibabu na huduma bora za afya . Masoko hayo yanatarajiwa kuwa dola za marekani bilioni 10.6 mnamo mwaka 2019 kutoa dola za marekani bilioni 2.8 mnamo mwaka 2014.

Masoko ya madawa ya India pia yanapata ukuaji muhimu kutokana na gharama mdogo na huduma bora . kuna makadiriyo kwamba sekta ya  afya inaongezeka asilmia 20 kila mwaka na itakuwa maradufu takriban dola za marekani bilioni 19 mpaka mwaka elfu mbili kumi na saba nchini India.