Myanmar imefungua mkutano wa amani na waasi wa kikabila

Kiongozi wa Myanmar Bi Aung San Suu Kyi na kamanda wa kijeshi wa nchi hiyo Jumatano walianza mkutano mkubwa na wawakilishi wa makundi ya wachache wa kikabila kujaribu kujaribu kuelekea amani ya kudumu baada ya miongo saba ya mahusiano yaliyoharibika na vita. Suu Kyi katika hotuba ya washiriki alisema, ana wasiwasi kuwa kuchelewa yoyote katika mkutano wa amani kunaweza kuathiri nafasi ya watu wake kupata amani.